Search This Blog

Saturday, May 17, 2014

Tiba ya Homa ya Dengue ukiwa nyumbani

 Tumia paracatemol hasa panadol na kunywa maji na juisi kwa wingi hasa juisi ya majani ya mapapai inapunguza makali sana ya homa hii kwani majani ya mapapai yanaongeza chembe za damu kwa haraka.
Homa hii wakati mwingine huitwa homa ya kuvunja mfupa(break bone fever) na imekuwepo miaka mingi na hasa nchi za kitropic zinapata wagonjwa wa dengue karibu kila mwaka wanaambukizwa watu wengi. Nchi nyingine nazo zinapata ugonjwa kila mwaka maambukizi yanakuwa kati ya 50 milioni mpaka 528 milioni duniani. Vifo ni kati ya 1%-5% bila tiba na tiba ikifanyika ya kuujua na kunywa maji kwa wingi na painkiller kama panadol ikatumika vifo ni chini ya 1%.

Dengue ni ugonjwa unaoambukizwa katika nchi zaidi ya 110 duniani.

Kinga ni kuharibu mazalio ya mbu na kuhakikisha tunaua mbu na kupiga dawa za kuharibu vyanzo vya mbu na kusafisha mitalo, kuondoa maji yaliyotuama na madampo kuchoma takataka hizo.

Ugonjwa huu unatokana na virus waitwao kitaalamu Flaviviridae; genus Flavivirus na wanatokana na mbu wa aina ya AIDES
 
Mbu na virus waenezao homa ya dengue


Huyu mgonjwa ana upele mgongo mzima kwa kusambaa na ni dalili mojawapo ya dengue

Dalili kuu za dengue ni:

  • Kichwa kisicho cha kawaida(kikali)
  • Homa
  • Kuumwa joint za mwili mzima na misuli
  • Kupata maupele kwenye ngozi mfano wa mapele ya surua
 Ugonjwa ukifikia kiwango fulani mgonjwa utoka damu puani na kufanana kama pressure imeshuka na kupungua chembe za damu mwilini na hapo mgonjwa anakuwa taabani sana.
 Tiba ya Homa ya Dengue
Mpaka sasa hakuna tiba rasmi wala chanjo, tiba yake ni kuhakikisha mwili una maji ya kutosha kwa kunywa maji salama kwa wingi na kutumia pain killers zile za kawaida tu kama panadol na kuhakikisha unakunywa sana ili ukojoe sana.

No comments:

Post a Comment