Search This Blog

Monday, October 8, 2012

Yahya A. S.kateme ashinda kwa kishindo kwenye Uchaguzi wa UVCCM Mkoa Kagera

 Yahya A S Kateme Mwenyekiti wa UVCCM mpya Mkoa Kagera akiwa anajibu hoja kwa makini. Ameshinda kwa zaidi ya  250% kila mtu anadai kuwa ni ushundi wa kihistoria Mkoani Kagera Kwa ngazi hii. Picha hii ya chini kushoto Yahya A S Kateme alikuwa ziarani Wilaya ya Misenyi na Nape Nauye Katibu wa NEC taifa mwezi may 2012

Uchaguzi uliofanyika jana tar 8/10/2012 wa kumchagua Mwenyekiti wa mkoa Umoja wa Vijana CCM mkoa wa Kagera umeenda vizuri ingawa dalili za kutoa rushwa zilikuwa zinaanza kuonekana baada ya kuona mambo yamekuwa mazito kwa baadhi ya wagombea. Udini nao ulianza kutumika kama kawaida ya baadhi ya washabiki wa wajumbe wenye kubagua wenzao kidini ili mradi wakidhi matakwa yao yatokanayo na woga wa kushindwa kwani mfa maji hakosi kutapa tapa, lakini yote haya hayakufua dafu kwenye nguvu ya mgombea Yahya A S Kateme aliyeonekana kushangiliwa na baadhi ya wajumbe hata kabla ya kupiga kura. Hii inatokana kijana huyu mtaalamu wa mambo ya Teknologia ya mawasiliano yaani ICT kuonyesha uongozi wake na jitihada zake kipindi alipokuwa Mwenyekiti wa Vijana wa wilaya mbili ya Kyerwa na Kayanga ikiwa wilaya moja ya karagwe kabla ya kugawanywa kuwa wilaya mbili kiasi kwamba juhudi zake za kuwaunganisha vijana wa ccm na kuwapa mbinu za kujikwamua kiuchumi kama kuanzisha SUCCOS ili iwasaidie kupata mitaji na kubuni miradi ya kuwakawamua na hatimaye waelekee kwenye kujiajiri kama yeye anavyojiajiri. Uchapakazi wake umejulikana hata kwa vijana wa wilaya zingine za Mkoa Kagera na kuamua kuwa lazima awe Kiongozi wa Mkoa ili chachu zake za kimaendeleo zisambae hata kwa vijana wa wilaya zote za Mkoa wa Kagera ndipo wameamua kumpa kura za kumwaga naye amepata kura 433 na aliyemfuata mpinzani wake Mkubwa Bwana Wilbroad kupata kura 192 na watatu kupata kura 1 hii inaonyesha alivyomzidi zaidi asilimia 250(250%) na ni ushindi wa kishindo katika Tanzania kushinda kwa asilimia hizi na hii ni kweli vijana wametaka mawazo mapya ya ubunifu na siyo bra bra za wanaotaka vyeo tu na baada ya kupata wanasahau ahadi zao na wanabaki kwenye kufitini wenzao na kuendeleza udini na ukabila. Mwenyekiti huyu mpya wa UVCCM Kagera, Yahaya A S Kateme mambo ya udini na ukabila kwenye siasa anayapiga vita na kuamini kuwa siasa ni kuwatumikia watu wote bila kubagua mtu yoyote ili mradi uadilifu na kanuni za utendaji kazi zimezingatiwa kwa mujibu wa Chama na Serikali.

N