Search This Blog

Thursday, May 8, 2014

Kazi na utapeli, kuwa makini na matangazo ya kazi

Duniani ya sasa hizi mbwa au paka anaweza akawa muaminifu kuliko mwanadamu ambao kapewa ziada ya utambuzi, siku kuna utapeli wa aina nyingi na kila siku unaongezeka na kufanya watu wasijue ipi taarifa ya kweli na ipi si kweli. Hii inasababisha kuwa na kasi ndogo katika maamuzi na kufanya maendeleo ya kweli yaweze kufikiwa mapema, siku hizi kuna matangazo mengi ya kazi na kubandikwa miji mikuu yakitaja mishahara itakayolipwa na bila kutaja ofisi iliko na uhalali wa ofisi, ila tu inawekwa namba ya siku ya mkononi.

Sasa utapeli huu unaanzia kwenye kupiga simu na hapo unapewa Lugha nzuri na mikakati ya kupata kazi na mwisho unatapeliwa, kuna jamaa walisoma tangazo la kazi kuwa ni kuajiriwa mgodi mmoja wa hapa Tanzania na wakaweka nafasi nyingi za kuajiriwa katika Tangazo na wakabandika miji mbali mbali hapa Tanzania. Jamaa wakachukua namba za simu wakaongea na mtu anayejiita Afisa Utumishi na akawamia watume maombi kwa email basi jamaa wakafanya hivyo na akawajibu kwa simu kuwa ameyapokea na akasema wametuma maombi wengi lakini atawaasaidia.

Wakawa wanaongea naye kwa simu na baadaye akawambia majina yao yamepitishwa waje kwenye interview na akawambia ili siku hiyo aweze kuwasaidia watume shs 45,000/= tu kwa Mpesa. Basi wakazituma na akasema nimezipokea mje kwenye interview siku fulania na saa fulani.

Jamaa wakafurahi na wakachukua usafiri mapema sana na kuelelekea kwenye interview, hii safari ilikuwa ndefu kwa hiyo ilibidi waondoke siku moja kabla ya interview ili wasichelewe na wakakosa kazi kwani wameisha kuwa na urafiki na Afisa Utumishi, walipofika karibu na Gate kuu ya Mgodi kwa sababu ya ulimzi mkali wakampigia simu kama alivyowambia kuwa mkikaribia mniambie nije niwapokee getini, basi wakapiga simu na akapokea na kuwapa pole na safari na kuwaeleza namna ya kujibu maswali ya interview na akawambia kuna wenzangu muhimu kwenye panel ya interview kwahiyo watume Lakini moja ya Tanzania(100,000/=) ili nao wagawane na hii moja kwa moja watakuwa wamepata kazi kwani hao wamo kwenye interview na yeye yumo.

Jamaa hawa walikuwa hawana pesa na wakamwambia sasa hivi tuna nauli tu ya kurudi na pesa yote imeisha na ndo maana wanatafuta kazi, jamaa akasema jitahidi kuwapigia jamaa, ndugu, marafiki wawatumie kwenye Mpesa hapo na nyie mnirushie kwenye simu yangu sasa hivi kwani muda wa Interview imebaki muda kidogo kuitwa kwenye ukumbi, jamaa kusikia hivyo wakaanza kuwapigia ndugu na jamaa kuwa tuko mgodini tumepata kazi kuna laki moja inatakiwa sasa hivi nisadie nitakurudishia na kukupa shukurani kwani mishahara iko juu na nikianza kazi mambo yatakuwa sawa hata wewe ndugu yangu na mwingine akampigia kaka yake mwenye duka na kumwambia nikope kaka hiyo duka nitaijaza mali nikilipwa mshahara wa kwanza kwani ninakaribia kupewa mkataba wa kazi.

Kwa lugha hizi jamaa wakatumiwa pesa kwa Mpesa na wao wakamrushia Afisa Utumishi Hewa wa Mgodini wasiyemjua kwa sura wala kama yupo, basi wakamuuliza na akasema nimepata na hapo ndipo akasema nakuja kuwachukua getini, jamaa wakaanza kujicheki kama wako smart na kuchomekea vizuri nguo na kupangusa viatu vyao ili akija kuwapeleka waende wakiwa smart.

Wakasubiri ikapita dakika 15 mpaka nusu sasa na wakampigia ili wamuulize yuko wapi labda amewakosa, maskini simu inasema namba hii haipatikani kwa sasa, labda mtandao tuma meseji na baadaye piga tena hakuna simu hewani, basi wakasubiri masaa 2 na kupiga tena simu inasema hii simu haipatikani, hawa wote wasomi kumbuka na wamepitia form six na vyuo tena vya sayansi.

Wakaamua wasogee getini na hali ya kuwa wanaogopa wasije wakaitwa wezi lakini wakaamua kumuita mlinzi mmoja kumtaka msaada wa taarifa, wakamuuliza kuwa hapa kuna interview ya kazi na wao wamekuja kwenye interview na Afisa Utumishi wamemsubiri ili kuwapeleka simu yake haipatikani! Mlinzi akawambia hapa hakuna interview na wala hakuna Tangazo la kazi la hivi karibuni na hawajaanza kuajiri tena.

Basi ndipo walihisi wanataka kuzimia na wakaondoka kimya kimya bila kuzidi kumpa story kamili mlinzi huyo na hali wana madeni na nauli imepungua na ahadi walizotoa kwa ndugu zikawa zinawarudia kichwani na kuwafanya wapate mfazaiko mkubwa.

Mimi na wewe tuwe makini katika kupokea na kufanyia kazi taarifa na habari yoyote hasa za kifedha kwa makini kwani hali si nzuri mtaani na hii haina cha Mzee. Kijana na wala Bosi wa Kampuni. Chunguza kwa kina kabla ya kukubali taarifa utakayopata.

NAFASI ZA MASOMO
JOOMLA CMS
GIS
TALLY
PASTEL
MYOB
COMPUTER REPAIR and MAINTENANCE

Contacts:
Email: tibaherbs@gmail.com 

 +255764041507/+255717147649

Dar es Salaam, Tanzania.






No comments:

Post a Comment