Search This Blog

Sunday, May 4, 2014

Sheikh Ilunga kapungu Afishwa saa 5 Usiku tar 4/5/2014

Inna Lillah Wainna Ileiy Rajiun
Picha ya  Marehemu Sheikh Ilunga Kapungu katika uhai wake



Sheikh Ilunga amefishwa saa 5 Usiku tarehe 4/5/2014 na Mazishi yatafanyika Makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni baada ya Alasiri katika Msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam.


Sheikh Ilunga alikuwa mwanaharakati katika kufikisha ujumbe kwa wanadamu kuhusu Mwenyezi Mungu na kumtii yeye peke yake katika Ibada, alikuwa anahamasisha maendeleo ya waislam kama kujenga shule na hospitali.

Sheikh Ilunga alikuwa anazunguka sehemu mbali mbali tanzania kuwazindua waislam kuhusu dhulma zidi yao kama kufanyiwa juhudi za ubaguzi katika elimu na kazi, hii alijitahidi kuwapa elimu waislam na watanzania wenye nia njema kuhusu mfumo kristo na bahati nzuri Alhamdulillah technologia imesaidia kufikisha ujumbe kwani hotuba zake ziko kwenye DVD, CD na kwenye Youtube kwenye internet. Yeye amefishwa lakini kazi yake ya kufikisha ujumbe na kuelimisha wanaodhulumiwa kwa mfumo wa siri usiokuwa rahisi kuugundua kwa mtu wa kawaida bado inaendelea kupitia Digitali.

Mwenye Mungu amsamehe na tuzidi kumuombea na sisi tutarejea kwa Mwenyezi Mungu muda wowote kuanzia sasa. Tujitahidi kufanya mema na kuomba msamaha, kutoa sadaka kabla ya kufishwa.

No comments:

Post a Comment