Search This Blog

Friday, April 20, 2012

Wabunge wachachamaa nchini Tanzania dhidi ya Ufisadi wa wazi

Wabunge waliopewa dhamana ya kuwakilisha wananchi katika maamuzi yao sasa wazidi kuwa wachungu dhidi ya baadhi ya mawaziri wanaodhihirisha utendaji wao kutokuwa makini katika ripoti za kamati mbalimbali.

Jana tarehe 19/4/2012 Mheshimiwa Zito Kabwe na wabunge wengine wameamua kupendekeza uwepo mchakato wa kupiga kura za kutokuwa na imani na waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda iwapo kufikia jumatatu mawaziri watano wenye matatizo ya kiufisadi katika wizara zao hawatajiuzulu basi waziri Mkuu atawajibishwa na bunge kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Hii inadhihirisha kuwa wabunge sasa wannafanya kazi ya kulinda masilahi ya wananchi waliowatuma bungeni na siyo kukumbayia watu wenye fikra za kuharibu bila kuwajibishwa.

Chama tawala kisifikiri wananchi wamesinzia kama muda wote wanapata rais kutoka CCM sasa wasipoangalia waweza kupata Rais bila wabunge au wakakosa vyote yaani wabunge na Rais, hii hali inaoneka katika uchaguzi huu wa mwaka 2012 wa kurudia baadhi ya majimbo CCM imeshindwa viti vyote kwa mpigo na hii inaonyesha picha wazi kuwa tunapoolekea mambo yatakuwa magumu kwa CCM. Nawapa ushauri viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutawala nchi hii watunze heshima yao kwa kutekeleza wajibu wao na kutumia mali ya nchi kwa uadlifu ndipo hali itakuwa nzuri kwao na wananchi kwa ujumla.

KOZI MUHIMU


Pata mafunzo ya Computer repair maintenance, Web site designing-JOOMLA, GIS, TALLY, MYOB, PASTEL na Programming



Contacts:
Email: computces@gmail.com 

 +255764041507/+255717147649

Dar es Salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment